Kuundwa kwa serikali ya umoja wa kitaifa Visiwani Zanzibar
Spika wa baraza la wawakilishi visiwani Zanzibar, Pandu Ameir Kificho amesisitiza kwamba kura ya maoni itakayoamua kuundwa kwa serikali ya umoja wa kitaifa Zanzibar itafanyika kabla uchaguzi mkuu.
Alisema chama tawala cha CCM hakiwezi kubatilisha uamuzi uliopitishwa na baraza hilo la wawakilishi. Josephat Charo amezungumza na Bwana Kificho na kwanza kumuuliza juu ya uwezekano wa serikali ya umoja wa kitaifa kuundwa kabla ya kufanyika uchaguzi mkuu nchini Tanzania.
Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com