KINSHASA:Mapigano yazuka kati ya Uganda na DR | Habari za Ulimwengu | DW | 26.09.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

KINSHASA:Mapigano yazuka kati ya Uganda na DR

Raia sita wa Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Kongo wameuawa na wengine watano wamejeruhiwa kufuatia mapigano kati ya majeshi ya Uganda na ya Kongo katika eneo la Ziwa Albert ambako kumegunduliwa mafuta.

Msemaji wa jeshi la Umoja wa Mataifa katika eneo hilo Gabriel de Brosses amesema kuwa mapigano hayo yalitokea siku ya jumatatu mchana kati ya askari wa nchi hizo.

Mapema msemaji wa jeshi la Uganda alisema kuwa askari wawili wa jeshi la kongo na mmoja wa Uganda waliuawa katika mapigano yaliyotokea kwenye eneo la maji ya Uganda.

Nchi hizo mbili zilitiliana saini makubalino mwanzoni mwa mwezi huu nchini Tanzania ya ushirikiano katika utafutaji na uchimbaji wa mafuta kwenye eneo la ziwa Albert.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com