KINSHASA : Shambulio lauwa 2 na kujeruhi 20 Congo | Habari za Ulimwengu | DW | 20.05.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

KINSHASA : Shambulio lauwa 2 na kujeruhi 20 Congo

Waasi wanaotuhumiwa kuwa wa Rwanda wameuwa watu wawili na kujeruhi wengine 20 katika shambulio mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo hapo jana ikiwa ni dalili mpya kabisa kwamba juhudi za amani nchini humo zinazoungwa mkono na Umoja wa Mataifa zinasambaratika.

Shambulio hilo kwa gari la mizigo la raia katika jimbo la vurugu la Kivu Kaskazini inaaminika kuwa limefanywa na waasi wa kundi la Vikosi vya Demokrasia kwa Ukombozi wa Rwanda FDLR ambalo linadhibitiwa na Wahutu huko mashariki ya Congo.

Shambulio hilo limetokea katika mji wa Katwiguru ulioko kilomita 100 kaskazini mwa mji mkuu wa jimbo hilo wa Goma.

Waliouwawa ni mwanajeshi mmoja na raia mmoja na miongoni mwa watu 20 waliojeruhiwa watatu wako mahtuti.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com