Kinshasa. Kundi la kutetea haki za waandishi lataka mwandishi afunguliwe jela. | Habari za Ulimwengu | DW | 21.05.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Kinshasa. Kundi la kutetea haki za waandishi lataka mwandishi afunguliwe jela.

Kundi la kutetea haki za waandishi habari, waandishi wasio na mipaka RSF, leo limetoa wito wa kuachiliwa huru kwa mwandishi habari wa Congo ambaye alikamatwa miezi sita iliyopita na amesahaulika katika jela mjini Kinshasa.

Katika taarifa iliyotumwa kwa shirika la habari la AFP, shirika hilo limetaka kuachiliwa huru kwa Bosange Mbaka , mwandishi anayefanyakazi na gazeti la mjini Kinshasa la mambenga.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com