Churkin akumbukwa na wengi umoja wamataifa
21 Februari 2017Churkin aliyebobea katika maswala ya demokrasia ya nchi za magharibi alipelekwa hospitali, ambako alifariki siku hiyo hiyo , siku moja tu kabla ya kutimiza miaka 65.
Watu wengi hususan viongozi wa nchi mbalimbali na wajumbe wa Umoja wa mataifa wamekuwa wakiomboleza kifo cha balozi Churkin.
Churkin alikuwa mjumbe wa Urusi wa Umoja wa mataifa kuanzia 2006 na mjumbe wa muda mrefu katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa .
Katibu mkuu wa umoja wa mataifa, Antonio Guterres alimpongeza Churkin na kusema kuwa alikuwa ni mwana diplomasia aliyebobea. "Balozi Churkin alitumikia wizara ya mamabo ya njee ya Urusi kwa njia nzuri na ya kipekee alipokuwa akipambana na migogoro migumu na mirefu ya historia ya hivi karibuni." Alisema Guterres
Pia raisi wa Urusi Vladimir Putin alimpongeza Churkin kwa kipaji chake na ujuzi na utaalamu aliokuwa nao.
Wanadiplomasia kutoka sehemu mbalimbali waliomboleza kwa kusema kuwa Churkin alikuwa bigwa katika kazi yake na pia alikuwa ni mtu aliyekuwa akipenda kazi yake pamoja na kutekeleza majuku majukumu yake . Churkin alikuwa pia ni msomi aliyebobea na alikuwa na shahada ya juu ya PHD katika somo la historia, lakini pia utotoni alikuwa ni muugizaji mzuri wa kuchekesha.
Churkin akumbukwa na wengi
Samantha Power aliyekuwa balozi wa Marekani katika umoja wa mataifa chini ya utawala wa Barack Obama aliandika katika mtandao wa kijamii wa twitter na kusema kuwa Churkin alikuwa mtu aliyebobea "kidplomasia na aliyejali sana sana watu". Aliendelea kuandika kuwa Churkin alijaribu wakati wote kusawazisha mivutano baina ya Marekani na Urusi kwa kadiri ya uwezo wake.
Kifo cha Churkin kimetokea katika wiki ambazo Urusi inajipanga na mkutano wa Umoja wa mataifa na jumuiya ya kimataifa, pia wakati huo huo uteulewa mpya wa viongozi mbalimbali katika ikula ya White house na juu ya hayo pia kuna mazungumzo ya Syria na Urusi.
Balozi wa Uingereza ndani ya umoja wa mataifa , Matthew Rycroft alimwita Churkin kuwa ni "gwiji la wadiplomasia na mtu mwenye tabia nzuri."
Churkin alijitokeza kuwa sura mpya katika masuala ya wizara ya nje hapo mwaka 1986 enzi za Urusi ya zamani ilipokuwa bado muungano ikiitwa Jamhuri za Kisovieti, alipotoa ushahidi dhidi ya Marekani.
Churkin pia aliwahi kuwa balozi wa Ubelgiji na Canada.
Katika mahojiano na kituo cha matangazo ya televisheni cha na RussiaToday Churkin alisema kuwa diplomasia siku hizi imekuwa ni "kazi ngumu" huku migogoro ya kisiasa ikiendelea na wakati huohuo kukiwa na hali ya utulivu.
Mwandishi : Najma Said/APE
Mhariri : Mohammed Abdul-Rahman