1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KIEV:Yulia Timoshenko asema kutakuwa na mizengwe uchaguzi wa Septemba

27 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBVc

Kiongozi wa upinzani nchini Ukraine Yulia Tymoshenko amezungumzia wasiwasi wake juu ya uchaguzi ujao wa bunge.

Amesema anaamini kwamba uchaguzi huo wa mapema utakabiliwa na mizengwe.

Tayari maafisa wa uchaguzi wamejaribu kukizuia chama chake kugombea kwenye uchaguzi huo.

Uchaguzi huo wa mwezi septemba umeitishwa baada ya kuwepo kwa mivutano ya kung’angania uongozi kati ya rais na waziri mkuu Viktor Yanukovych.

Tymoshenko amesema anawasiwasi kwamba uchaguzi huu hautakuwa huru na wa haki kwa sababu sheria zilizokuweko za kujaribu kuzuia udanganyifu katika upigaji kura zilibadilishwa hivi karibuni na maafisa wa uchaguzi.

Waangalizi wa kimataifa pia wamezungumzia mashaka yao kuhusu uchaguzi huo.