1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KHARTOUM:Vigogo wazuru Darfur na kutaka vikosi vifike haraka

4 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7Ih

Kundi la vigogo wa zamani likongozwa na mshindi wa Nobel Desmond Tutu linatoa wito kwa kikosi kilichoimarishwa cha kulinda amani kupelekwa Darfur haraka iwezekanavyo kufuatia mauaji ya wanajeshi 10 wa Umoja wa Afrika wa kulinda amani.

Hii ni mara ya kwanza kwa kundi hilo lililoanzishwa na rais mstaafu wa Afrika Kusini Nelson Mandela na mkewe Graca Machel na Bwana Desmond Tutu na kuwahusisha pia mjumbe wa Umoja wa mataifa wa zamani Lakhdar Brahimi pamoja na rais mstaafu wa marekani Jimmy Carter.

Kundi hilo lilizuru eneo la Darfur siku ya jumapili ili kushuhudia wenyewe namna wakazi wanavyoteseka kufuatia vita vilivyosababisha vifo vya takriban watu laki 2.

Viongozi hao walikutana na Rais wa Sudan Omar el Bashir na kufanya mazungumzo na wanachama wa uongozi wa Juba ulio mji mkuu wa eneo la kusini mwa Sudan ililo na uwezo wa kujisimamia.

Mazungumzo ya amani yanapangwa kufanyika mjini Tripoli, Libya tarehe 27 mwezi huu na kuhusisha makundi ya waasi wa Darfur na serikali ya Sudan ili kumaliza ghasia.