1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KHARTOUM: Rais al-Bashir na Kiir washindwa kuafikiana

19 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7Ee

Majadiliano yaliyolenga kutenzua mgogoro wa serikali ya mseto ya Sudan yamemalzika bila ya mapatano.Rais wa Sudan,Omar al-Bashir alishindwa kupata imani ya Naibu-Rais,Salva Kiir aliejitoa serikalini ambae pia ni kiongozi wa Sudan ya Kusini.

Juma lililopita,chama cha Kiir cha SPLM kiliwatoa mawaziri wake kutoka serikali ya mseto. Chama hicho kimelalamika kuwa masuala muhimu katika mkataba wa amani uliotiwa saini mwaka 2005 hayakutekelezwa.Pande hizo mbili,zinatazamia kukutana tena siku ya Jumatatu.