KHARTOUM: Muakilishi maalum wa Umoja wa mataifa nchini Sudan aelekea New York | Habari za Ulimwengu | DW | 24.10.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

KHARTOUM: Muakilishi maalum wa Umoja wa mataifa nchini Sudan aelekea New York

Muakilishi maalum wa Umoja wa mataifa nchini Sudan, Jan Pronk, ameondoka kutoka Sudan baada ya serikali ya Sudan kumtaka afanye hivyo. Pronk alifukuzwa kutoka Sudan baada ya kuandika katika mtandao wake binafsi kuwa jeshi la ´serikali ya Sudan lilishindwa katika mapigano katika jimbo la Drafur, magharibi mwa Sudan na kwamba limevunjika moyo. Jan Pronk ambae kwa sasa yuko jiani kuelekea mjini New York, atakuwa na mashauriano na Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa, Kofi Annan. Msemaji wa Umoja wa mataifa, Stephanne Dujarric, amesema Kofi Annan ana imani kubwa na Bwana Jan Pronk. Dujarric amehakikisha kuwa mpango wa Umoja wa mataifa kuhusu Sudan, hujabadilika:

´´Jukumu letu ni kuona mkataba wa amani ukitekelezwa kamili katika eneo la kusini. Jukumu letu kuhusu hali ya mambo katika jimbo la Darfur bado ni lile lile. Jan Pronk bado ndie muakilishi wetu. Yuko njiani kuelekea New York. Atakuwa na mazungumzo na Katibu mkuu yuko tayari kumsilikiza´´.

Hadi sasa Sudan imepinga kutumwa nchini humo kikosi cha wanajeshi wa Umoja wa mataifa 20,000 kuchukuwa nafasi ya wanajeshi 7,000 kutoka Afrika. Inakisiwa kuwa watu 200,000 waliuawa na wengine milioni 2,5 kulazimika kuyahama maskani yao kwa muda wa miaka mitatu ya mzozo katika jimbo la Darfur kati ya waasi na wanamgambo tiifu kwa serikali.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com