KHARTOUM: Juhudi za amani Darfur kuanza | Habari za Ulimwengu | DW | 08.01.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

KHARTOUM: Juhudi za amani Darfur kuanza

Juhudi mpya za Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa za kuanzisha mazungumzo ya amani kati ya waasi wa Darfur na serikali ya Sudan zinakabiliwa na kikwazo kikubwa.

Mazungumzo hayo yanatarajiwa kuanza baadaye mwezi huu na mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa Jan Eliasson alitarajiwa kuwasili leo mjini Khartoum kuanza maandalizi.

Mustafa Osman Ismail, ambaye ni mshauri wa rais wa Sudan, amesema ipo haja ya kuwajumulisha viongozi wa waasi katika mazungumzo hayo. Eneo la Darfur limeendelea kushuhudia vita huku mahakama ya kimataifa ya jinai mjini The Hague Uholanzi ikisema serikali ya Sudan haina ushirikiano wa kuwawasilisha watuhumiwa wa mzozo huo.

Muongoza mashtaka mkuu wa mahakama hiyo, Luis Moreno- Ocampo amesema,´Kwa mujibu wa sheria iliyopo, Sudan haina jukumu la kushirikiana na mahakama ya jinai ya kimataifa kwa sasabu si mwanachama na wala haikuidhinisha sheria hiyo. Iwapo Sudan itaitambua sheria hii basi itakuwa na jukumu lakini mpaka sasa serikali haijasema kama inaitambua.´

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com