Khartoum. Chad yakabiliwa na maafa iwapo wakimbizi kutoka Darfur wataendelea kwenda huko. | Habari za Ulimwengu | DW | 23.12.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Khartoum. Chad yakabiliwa na maafa iwapo wakimbizi kutoka Darfur wataendelea kwenda huko.

Kamishna wa umoja wa mataifa wa haki za binadamu ameonya kutokea maafa ya kibinadamu nchini Chad iwapo wakimbizi kutoka katika jimbo la jirani la Darfur nchini Sudan wataendelea kukimbili nchini humo.

Ziara ya kamishna huyo inakuja wakati serikali ya Sudan inatoa ishara kuwa huenda ikakubaliana na uwekaji wa jeshi la umoja wa mataifa la kulinda amani katika jimbo la Darfur. Kamishna Antonio Gueterres amesema kuwa anaikaribisha hatua hiyo.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com