Khartoum: Bashir aukataa tena mpango wa Umoja wa mataifa kuhusu Darfur | Habari za Ulimwengu | DW | 28.11.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Khartoum: Bashir aukataa tena mpango wa Umoja wa mataifa kuhusu Darfur

Rais Omar Hassan al-Bashir wa Sudan amelikataa tena jaribio la Umoja wa mataifa kutuma wanajeshi wa kulinda amani katika jimbo la Sudan la Darfur. Kiongozi huyo aliliita tangazo la Katibu mkuu wa umoja huo Kofi Annan mjini Addis Ababa wiki mbili ziliopita, kwamba Sudan imekubali mpango wa ubia wa jeshi la pamoja kati ya umoja wa mataifa na umoja wa Afrika kwa ajili ya Darfur kuwa ni uwongo. Kwa karibu miaka minne sasa, wanamgambo wenye asili ya kiarabu na wanaoungwa mkono na Serikali-Janjaweed-wamekua wakipigana na waasi katika jimbo hilo. Mashirika ya misaada yanakadiria kwamba kiasi ya watu 200,000 wameuwawa na zaidi ya milioni 2,5 kulazimika kuyakimbia makaazi yao.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com