Kenya kujiunga na AMISOM | Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili | DW | 17.11.2011
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Timu Yetu

Kenya kujiunga na AMISOM

Serikali ya Kenya imetangaza kuwa ipo tayari kuwatuma wanajeshi wake kujiunga na kikosi cha kulinda amani nchini Somalia cha Umoja wa Afrika, AMISOM

default

Wanajeshi wa Kenya nchini Somalia,

Hii ni hatua inayojiri mwezi mmoja baada ya jeshi lake kuanzisha operesheni dhidi ya wanamgambo wa Al shabaab katika nchi hiyo yake jirani.

Militär in Kenia Afrika

Haijajulikana iwapo waliopo kusini mwa Somalia watajiunga na kikosi hicho cha AMISOMKufutia mkutano uliofanyika hapo jana kati ya rais Mwai Kibaki wa Kenya, rais Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda na rais wa serikali ya mpito nchini Somalia waliokutana katika ikulu ya Nairobi, Rais kibaki ametoa taarifa hapo jana na kusema kuwa viongozi wenzake hao waliikaribisha hatua ya Kenya kujitolea kukiimarisha kikosi cha AMISOM kilichopo Somalia.

Ujumbe huo wa kulinda amani ambao kwa hivi sasa unajumuisha wanajeshi 9700 wanaotoka Uganda na Burundi pekee una jukumu la kuilinda serikali ya mpito Somalia inayoungwa mkono na mataifa ya mgharibi dhidi ya wanamgambo hao wa Al shabaab.

Hatahivyo taarifa hiyo haikueleza iwapo vikosi vya kenya vilivyopo tayari kusini mwa Somalia vitajumuishwa katika kikosi hicho cha AMISOM na pia haikuelezea iwapo mchango huo wa Kenya utajumuisha kikosi cha kando kipya cha wanajeshi.

Taarifa hiyo ilieleza kuwa wanajeshi wanaopigana nchiniSomalia pamoja na wanajeshi wa aserikali yampito nchini humo wanatoa nafasi nzuri ya kihistoria kwa eneo hilo ya kurudisha utulivu na usalama Somalia.

Viongozi hao watatu walisisitiza haja ya kushinikiza ushirikiano katiya jeshi la AMISOM na jeshi la serikali ya mpito Somalia na vikosi vya ulinziu vya Kenya ili kufanikiwa kupambana nkundi hilo la kigaidi la Al shabaab.

Horn von Afrika Hungersnot

wakati huohuo Rais kibaki aligusia kuwa Djibouti pia ilijitolea kutoa wanajeshi wake kwa AMISOM, hatua iliyokaribishwa na viongozi hao katika mkutano huo wa jana.

Walito wito kwa nchi nyingine za Afrika zilizoahidi kuchangia wanajeshi katika kikosi hicho cha kulinda amani Somalia kutimiza kwa haraka ahadi zao.

Sierra Leone iliahidi mnamo mwezi Agosti kutuma wanajeshi kiasi ya 850 baada ya mwezi Aprili mwaka ujao.

Umoja wa Afrika umekuwa ukitoa wito wa kutumwa haraka wanajeshi 3000 zaidi baada ya kutolewa idhini na Umoja wa matiafa mwaka uliopita, hususan baada ya kundi hilo la Al shabaab kuondoka katika mji mkuu unaokumbwa na mapigano Mogadishu.

Horn von Afrika Hungersnot

Hoteli iliyoripuliwa mjini Mogadishu katika mapigano

Haya yanajiri wakati hii leo mjini Addis Ababa baraza la amanina usalama la Umoja huo wa Afrika linakutana kujadili njia za kuimarisha ujumbe wake nchini Somalia katika jitihada za kuiimarisha nchi hiyo.

Vikosi vya AMISOM vimekuwa vikipigana na Al shebaab lililo na mafungamano na kundi la kigaidi la Al qaeda kwa miaka minne mjiniMogadishu lakini kwa sasa vimetawanyika nje ya mji mkuu huo.

Mwandishi: Maryam Abdalla/Afp/Afpe

Mhariri:Josephat Charo

 • Tarehe 17.11.2011
 • Shirikisha wengine Tuma Facebook Google+
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo http://p.dw.com/p/13CI9
 • Tarehe 17.11.2011
 • Shirikisha wengine Tuma Facebook Google+
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo http://p.dw.com/p/13CI9

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com