Katiba Mpya: Wanasheria Zanzibar wasema serikali imevunja Katiba | Matukio ya Afrika | DW | 12.06.2012
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Afrika

Katiba Mpya: Wanasheria Zanzibar wasema serikali imevunja Katiba

Baraza la Wawakilishi la Zanzibar linapokea Sheria Na. 8, 2012 iliyopitishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kusainiwa na Rais Jakaya Kikwete juu ya kuanzishwa Tume ya Maoni ya Wananchi kwa Katiba Mpya.

Viongozi wakuu wa Zanzibar na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Viongozi wakuu wa Zanzibar na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kitendo cha Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuwasilisha Sheria Na. 8, 2012 iliyopitishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kusainiwa na Rais Jakaya Kikwete juu ya kuanzishwa Tume ya Maoni ya Wananchi kwa Katiba Mpya wakati hata Tume yenyewe imeshaapishwa na kuanza kazi, kinalalamikiwa na wanaharakati wa sheria, wakisema kwamba kinakiuka utaratibu wa kikatiba.

Mohammed Khelef amezungumza na mwanasheria wa Kituo cha Haki na Sheria cha Zanzibar, Is-hak Sharif, ambaye kwa sasa yuko safarini London, Uingereza, kujua kwa nini wanasheria waanaamini kuwa Katiba imevunjwa. Kusikiliza mahojiano hayo, tafadhali bonyeza alama ya spika za masikioni hapo chini.

Mahojiano: Mohammed Khelef/Is-haq Sharif
Mhariri: Othman Miraji

Sauti na Vidio Kuhusu Mada