1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Karachi. 40 wafariki kutokana na mvua kubwa.

24 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBox

Wafanyakazi wa uokozi kusini mwa Pakistan wanasema kuwa kiasi watu 40 wameuwawa na wengine kadha wamejeruhiwa kutokana na mvua kubwa ambazo zimesababisha kung’olewa kwa miti pamoja na mabango makubwa ya matangazo ya biashara.

Wengi wa waliofariki ilikuwa ni kutokana na kuanguka kwa mapaa ya nyumba na kunaswa na umeme mjini Karachi.