1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kanzela Merkel na msukosuko wa fedha

15 Oktoba 2008

Kanzela wa Ujerumani amehutubia Bunge leo juu ya mpango wa kuyaokoa mabenki na athari zake kwa uchumi wa Ujerumani .

https://p.dw.com/p/FaWT
Angela MerkelPicha: AP

Kwa muujibu wa Kanzela Angela Merkel wa Ujerumani,uchumi wa dunia unakabiliana na mtihani mkubwa kabisa wakati huu tangu ule wa miaka ya 1920.Wiki iliopita,masoko mashuhuri ya fedha na ya mikopo yalifikia hali ya kulemaa-alisema hii leo Kanzela Merkel katika taarifa yake mbele ya Bundestag-Bunge la ujerumani mjini Berlin.

"Imelazimika kwahivyo, kurejesha uwezo wa mabanki kuwa na akiba na raslimali pamoja na kuweza kuuza mali zilizo hatarini kufilisika.Isitoshe, Tume ya ulaya ,pengine hii hii leo, itarekebisha kanuni za masharti ya kushindana kibiashara na washirika wetu wa kimataifa.

Tumezungumzia swali hili sana siku chache zilizopita.Na ni jambo lenye umuhimu mkubwa kwamba, hatua zinachukuliwa ili mwishoni mwa robo ya tatu ya mwaka , muongozo mpya unafuatwa.Hii ni muhimu pia kwa uwezo wa kushindana kiuchumi wa Ujerumani."

Alisema Kanzela Merkel.

Kanzela Merkel akasema zaidi kwamba rasmi ya sheria inayapa mabenki dhamana ya hadi Euro bilioni 400 kama kiinua mgongo.Kutoa dhamana hiyo kwa serikali ya shirikisho ni hatua ya kuonesha imani kwa mabenki na kuyawezesha kutoa mikopo.

Dhamana hiyo imetenga kando kima cha Euro bilioni 20 kupambana na hatari zozote zitakazochomoza-hivyo nio kusema 5% ya kima kizima cha dhamana inayotolewa.

Kanzela wa ujerumani akataja sehemu ya pili muhimu ya hatua hizo inahusika na kuyapata mabanki raslimali za akiba za fedha .Mabenki yawe na uwezo kwa muda fulani kuweza kukopeshana.Msaada kama huo utatolewa tu ikiwa banki zitawajibika na zitafuata kanuni maalumu.Hii maana yake kufuata muongozo wa kuweka vikomo maalumu vya mishahara ya mameneja na posho lao-muongozo katika kuendesha shugbhuli za kibenki na katika kutoa mikopo na hasa kwa makampuni au viwanda vidogo na vya wastani pamoja kuishirikisha serikali katika faida zao .

Hatua nyengine muhimu aliozungumzia Bungeni leo kanzela Merkel na iliomo katika sheria inayopangwa kupitishwa ni kuiwezesha serikali ikihitajika kununua mabanki yanayoyumbayumba.Fedha zitakazovunwa kutokana na mauzo kama hayo, yarejee kuwanufaisha walipakodi. Mpango huu, lakini, alisema kanzela Merkel,utaepukwa kuchukuliwa mara kwa mara.

Mwishoe akasema:

"Mabibi na mabwana, niruhusuni niweke wazi kabisa:Hatari inayokabili utulivu katika masoko ya fedha, bado haikutoweka.Inatupasa lakini ,haraka kama iwezekanavyo ,kupitisha sheria hii ambayo inaweka msingi wa kutuliza mambo katika masoko ya fedha.Kwani, hii ni muhimu sana kwa kustaweisha uchumi na nafasi za kazi."