Kansela Merkel akutana na Waziri Mkuu wa Italia Prodi | Habari za Ulimwengu | DW | 21.11.2007
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Kansela Merkel akutana na Waziri Mkuu wa Italia Prodi

Suala la mustakbali wa Kosovo limehodhi mazungumzo kati ya Kansela Angela Merkel wa Ujerumani na Waziri Mkuu wa Italia Romano Prodi hapo jana.

Katika mkutano wao uliofanyika karibu na mji mkuu wa Berlin Merkel ametilia mkazo kuwepo kwa msimamo mmoja wa Umoja wa Ulaya kuhusu suala la jimbo hilo la Serbia.Prodi amesisitiza kuihakikishia serikali ya Serbia kwamba mustakbali wake uko katika Umoja wa Ulaya.Afghansitan pia ilikuwa juu kwenye agenda ambapo viongozi hao wote wawili wametowa wito wa kufanyika kwa mkutano mpya wa kimataifa wa juhudi za ujenzi mpya nchini humo.

Kwa mujibu wa duru za Italia mkutano huo unaweza kuwa na msingi kama ule wa mkutano wa mwaka 2006 mjini London ambao umechangisha euro bilioni 8.7 kwa ujenzi mpya wa Afghanistan .

 • Tarehe 21.11.2007
 • Shirikisha wengine Tuma Facebook Google+
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo http://p.dw.com/p/CPlt
 • Tarehe 21.11.2007
 • Shirikisha wengine Tuma Facebook Google+
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo http://p.dw.com/p/CPlt

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com