Kansela Merkel akabiliwa na mtihani wa kisiasa bungeni leo
29 Septemba 2011Matangazo
Kansela wa ujerumani, Angela Merkel, anakabiliwa na mtihani wa kisiasa leo wakati bunge litakapoupiga kura mfuko maalum wa fedha unaolenga kuzisaidia nchi zinazokabiliwa na madeni katika kanda inayotumai sarafu ya euro. Wabunge wa vyama vinavyounda serikali yake ya mseto walio na wasiwasi kuhusu Ujerumani kuisaidia Ugiriki kuondokana na tatizo la madeni, huenda wakapiga kura kuupinga mfuko huo wa thamani ya euro bilioni 440.
Kura za wabunge wa upinzani wanaounga mkono zitahakikisha Ujerumani inaridhia mfuko huo wa uokozi. Finland iliidhinisha kuongeza mchango wake katika mfuko huo hapo jana.