KANSAS:Kimbuga chaua watu tisa na kuusambaratisha mji | Habari za Ulimwengu | DW | 06.05.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

KANSAS:Kimbuga chaua watu tisa na kuusambaratisha mji

Watu tisa wamekufa baada ya kibunga kiitwacho Tornado kulikumba jimbo la kati la Kansas nchini Marekani.Mji wa Greensburg ndiyo uliyoathiriwa vibaya na kibunga hicho

Hali ya hatari imetangazwa na watu wamezuiwa kuendesha magari na kutakiwa kuondoka katika mji huo.

Kiasi cha wakazi elfu moja na mia sita wa mji huo walipata taarifa ya hadhari ya ujio wa kimbuka hicho dakika ishirini tu kabla ya kimbunga kuupiga mji huo.

Maafisa wa chama cha msalaba mwekundu huko Kansas wanasema kuwa asilimia 90 ya nyumba katika mji huo zimebomolewa na kimbunga hicho.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com