1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kampeni za uchaguzi zahanikiza magazetini

29 Januari 2013

Kampeni za uchaguzi zimehanikiza hata kabla ya kuanza rasmi.Zinaanzia pendekezo la waziri wa nishati na kufikia muungano uwe wa aina gani baada ya uchaguzi mkuu msimu wa mapukutiko ujao

https://p.dw.com/p/17TK8
Miambo ya kunasa nishati ya juwaPicha: dapd

Waziri wa nishati wa serikali kuu ya Ujerumani Peter Altmeier amependekeza bei ya nishati iwekewe kikomo ili isizidi kuongezeka.Wahariri wanajiuliza kwanini akatoa pendekezo hilo bila ya kushauriana na wenzake serikalini ?Gazeti la Lausitzer Rundschau linahisi:Pendekezo hilo si ufumbuzi,ni mchango wake tu katika kampeni ya uchaguzi.Ukweli umedhihirika kutokana na jinsi alivyolitoa pendekezo hilo.Angebidi kwanza azungumze na wengine badala ya kubuni mipango ya siri na kuitangaza baadae kwa fakhari mbele ya waandishi habari.Kinachohitajika haraka kwa kweli ni mageuzi ya kina ya sheria itakayoifanya nishati mbadala siku za mbele iweze kushindana kwa nguvu zaidi kuliko sasa,na ikiwezekana katika masoko yote ya Ulaya.Mageuzi hayo ya sheria hayatowezekana lakini katika wakati huu ambapo kampeni za uchaguzi zimehanikiza,pengine matokeo ya uchaguzi yatakapojulikana, msimu wa mapukutiko mwaka huu.Na wakati huo lazma mageuzi ya sheria yafanyike.

Gazeti la "Badische Neueste Nachrischten linashuku kama mageuzi hayo ya sheria yatafanyika.Gazeti linaendelea kuandika:"Kama pendekezo la Altmeier litatekelezeka,ajuaye Mungu.Wenye kupigania masilahi ya mashirika ya nishati wameshaanza kuingia mbioni kupinga bei ya nishati isiwekewe kikomo na upande wa upinzani nao unamtuhumu kuitumia nishati kwa masilahi ya kampeni za uchaguzi.Hata washirika serikalini FDP wanaonyesha kutoivalia njuga fikra hiyo.

Aina ya muungano baada ya uchaguzi

.
Washirika wa sasa serikalini:waziri wa mambo ya nchi za nje,Guido Westerwelle,waziri wa uchimi Philipp Rösler na kansela Angela Merkel (kutoka kushoto)

Karata za muungano wa aina gani uundwe baada ya uchaguzi mkuu,zimeshaanza kuchanganywa.Gazeti la "Reutlinger General-Anzeiger linaandika:" Wanamikakati katika makao makuu ya chama cha CDU mjini Berlin-Konrad-Adenauer-Haus wanakumbwa na kizungumkuti:Wajerumani,kwa mujibu wa uchunguzi wa maoni ya umma,wanamtaka Angela Merkel aendelee kuwa kansela,lakini hawautaki muungano wa vyama vya CDU/CSU naFDP.Wanaweza kupoteza madaraka wakiung'ang'ania muungano huo.Muhimu zaidi na ambalo linatoa picha ya hali halisi namna ilivyo katika medani ya kisiasa ni ule ukweli kwamba mabadiliko ya serikali katika jimbo la Lower Saxony yameufanya muungano wa CDU/CSU na FDP usiwe na nguvu hata kidogo katika baraza la wawakilishi wa majimbo-Bundesrat.Na hiyo ni sababu nyengine inayomfanya Angela Merkel aangalie pia upande wa SPD na pia ule wa walinzi wa mazingira Die Grüne.

Mursi ziarani Ujerumani

Ägypten Kairo Unruhen
Machafuko mjini CairoPicha: Getty Images

Na hatimae lilikuwa gazeti la Westfälische Nachrichten" lililoandika kuhusu ziara ya rais wa Misri,Mohammed Mursi nchini Ujerumani.Gazeti linaendelea kuandika:"Hatajisikia vizuri Angela Merkel,pale rais wa Misri,Mohammed Mursi atakapofika ziarani nchini Ujerumani.Watu kwa hivyo wasitegemee picha ya kuvutia:Nani anapendelea kupigwa picha akipeana mkono na muimla?Na zaidi ya hayo, ikiwa ghadhabu za umma katika mto Nil dhidi ya utawala wa Udugu wa kiislam hazipunguwi.Ikiwa matumizi ya nguvu yataigubika ziara ya rais huyo wa Misri mjini Berlin.Kipi Angela Merkel anaweza kumpatia mgeni wake......kama si kumpa mkono,kuamkiana.Kumpatia muimla misaada ya kiuchumi?Hasha.Anaweza kansela kumkumbusha jinsi haki za binaadamu zinavyoendewa kinyume na demokrasia kutoheshimiwa.Hilo litawafurahisha sana wananchi wa Misri na kuwapa moyo.

Mwandishi:Hamidou Oummilkheir/Inlandspresse

Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman