Kampeni za kura ya maoni kumalizika leo Kenya
2 Agosti 2010Matangazo
Kampeni za kuunga mkono na kupinga katiba mpya iliyopendekezwa nchini Kenya zinamalizika rasmi hii leo, ingawa hakutarajiwi kufanyika mikutano ya kusisimua. Jana upande unaoiunga mkono katiba mpya iliyopendekezwa ulikamilisha rasmi kampeni zake na leo upande unaopinga huenda ukawa na mkutano wake wa mwisho. Pande zote mbili, upande wa Ndio na Hapana, zina matumaini ya kushinda kura ya maoni kuhusu katiba hiyo itakayofanyika Jumatano wiki hii.
Mwandishi wetu Alfred Kiti kutoka mjini Naironi, ametuandalia taarifa hiyo.
Mwandishi:Alfred Kiti
Mhariri: Abdul-Rahman Mohamed