1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KAMPALA:Maelfu kukabiliwa na njaa baada ya mafuriko

10 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7H5

Shirika la chakula la umoja wa mataifa na shirika la kutoa misaada la Oxfam yameonya kwamba maelfu ya raia wa Uganda walioathirika kwa mafuriko ya hivi karibuni wanakabiliwa na hatari ya kukumbwa na njaa iwapo misaada ya chakula haitawafikia watu hao hivi karibuni.

Mkuu wa shirika la chaklula la umoja wa mataifa WFP Josette Sheeran amesema kwamba Uganda ni nchi mojawapo iliyokumbwa na mvua kubwa zilizosababisha mafuriko katika nchi zilizo katika eneo la jangwa la Sahara barani Afrika.

Kanda ya kaskazini mashariki mwa Uganda imeathirika zaidi na mvua hizo kubwa.

Takriban watu 300,000 wamepoteza makaazi yao hali kadhalika mashamba yao yalisombwa na mafuriko.