1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KAMPALA:Kundi la waasi la ADF mashariki ya Kongo kukabiliwa Ijumaa

28 Septemba 2005
https://p.dw.com/p/CEX4

Jeshi la Uganda limeonya kundi linaloshukiwa kuwa la waasi lililojificha mashariki mwa jamhuri ya kidemokrasi ya Kongo kujisalimisha au kukabiliwa na mashambulio ya kijeshi mwishoni mwa wiki.

Kufuatia hali ya wasiwasi juu ya kuwepo kwa wapiganaji waasi wa jeshi la Uganda LRA katika eneo hilo hilo,inasemekana kuwa wanachama wa kundi la waasi wa ADF Allied Demokratic Forces watakabiliwa iwapo hawatajisalimisha kwa hiari kufikia ijumaa ijayo.

Msemaji wa jeshi la Uganda Shaban Bantarizaamesema operesheni zozote za kulivamia kundi hilo zitafanywa na wanajeshi wa jamhuri ya kidemokrasi ya Kongo na wanajeshi wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani kufuatia ombi la rais wa Uganda Yoweri Museveni.

Kundi la ADF lilizuka mnamo mwaka 1996 kwa kuanza kufanya mashmbulio katika maeneo ya magharibi mwa Uganda kama sehemu ya juhudi za kuindoa madarakani serikali ya rais Kaguta Museveni na kuwepo kwao kulitumiwa na serikali ya Uganda kuvipeleka vikosi vyake vya kijeshi Zaire ya zamani.