1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KAMPALA : Polisi wapambana na waandamanaji

17 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CC9E

Polisi ya Uganda leo imetumia maji ya moto na mabomu ya kutowa machozi,virungu na risasi za moto kuwatwanya mamia ya wafuasi wa upinzani waliokuwa wakipinga kukamatwa kwa wanasiasa wawili wanaoshutumiwa kuchochea ghasia dhidi ya Wahindi.

Maafisa wa usalama wengi wakiwa katika mavazi ya kawaida walitumia nguvu kuwatawanya mamia ya waandamanaji waliokusanyika kuwaunga mkono wabunge wawili wa upinzani waliokamatwa kuhusiana na maadamano yaliofanyika hapo Alhamisi ambapo Muhindi mmoja na waandamanaji wawili wameuwawa.

Polisi iliwakamata wabunge Beatrice Atim na Hussein Kyanjo na watu wengine 25 hapo Jumatatu kuhusiana na maandamano ya ghasia mjini Kampala wiki iliopita kupinga mpango wa serikali wa kuuza theluthi moja ya msitu wa Mabira kwa kampuni inayomilikiwa na Muhindi kwa ajili kupanda miwa.