1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kalenda za michezo 2009

29 Desemba 2008

Mwaka wa Kombe la mashirikisho Afrika Kusini na ubingwa wa riadha Ujerumani:

https://p.dw.com/p/GOo8
Nembo ya DFB-shirikisho la dimba la Ujerumani.Picha: AP

Mwaka wa michezo 2008 umemalizika na mwaka wa michezo 2009 ukianza na kombe la vijana la Afrika Januari 18 huko Rwanda-halafu sherehe za kumtawaza rasmi "mchezaji bora wa dimba wa Afrika wa mwaka" mjini Dakar,Senegal hapo Januari 23.

Tunawakagulia mwaka wa Kombe la mashirikisho Juni ijayo nchini Afrika kusini-kombe litakalofungua pazia la Kombe la dunia 2010.

Na mbali na premier League-Ligi ya uingereza, tunawakagulia pia mwaka wa michezo Ujerumani ambao kilele chake ni mashindano ya ubingwa wa riadha ya dunia-world athletics championships mjini Berlin hapo August.

Wakati Bundesliga iko likizoni,Premier League-ligi ya uingereza iliendelea mwishoni mwa wiki licha ya siku kuu za X-masi.Liverpool ikiwa imefungua mwanya wa pointi 3 kileleni ikifuatwa na Chelsea iliopoteza pointi 2 ,Sir Alex Ferguson anaamini Manchester united iko njiani kutamba katika premier League mnamo nusu ya pili ya msimu huu.Hii inafuatia ushuindi wa Manu wa bao 1:0 dhidi ya stoke City.Ushindi huo umefufua matumaini ya Manu kuzipiku baadae Liverpool na Chelsea.

Liverpool iliilaza . Chelsea ilimudu sare 2:2 na Fulham wakati Arsenal iliilaza Portsmouth bao 1:0.Bao 1 la Mmisri Amr Zaki lilitosha kwa Wigan Athletic kuitimua nje Bolton Wanderers.

Ingawa Ujerumani itaandaa mashinda no ya ubingwa wa riadha wa dunia hapo August,sura ya michezo ya Ujerumani mwaka huu ujao si nzuri:

Jane Nyingi anaripoti:

Dola hili kuu la zamani la michezo imepungukiwa na mastadi katika medani mbali mbali za michezo-kuanzia kabumbu , riadha hadi hodhi la kuogolea ambam,o Ujerumani kwa desturi hutamba.

Miji ya Berlin na Leipzig imepatwa na mkosi katika juhudi zao za kutaka kuandaa michezo ya Olimpik miaka ya karibuni.

Mashindano makubwa kama vile yale ya Tennis ya Wimbledon hayatoneshwi tena katika TV zisizotoza ada na hakuna kinachoonekana kwa mashabiki yanapofanyika mashindano ya riadha ya Golden League,kwani kabumbu linatawala TV zote.

Stadi pekee maarufu wa dimba-nahodha wa timu ya taifa ya Ujerumani anaeichezea Chelsea ya uingereza, Michael Ballack ndie pekee katika ile orodha fupi ya wanaspoti bora wa mwaka 2009.Katrin Krabbe alikuwa mjerumani wa kwanza kushinda taji la riadha la dunia hapo 1991 na majogoo wa Ujerumani katika medani ya Tennis akina Boris Becker na Steffi Graf, zamani wametoweka.

Katika michezo ya Olimpik iliopita huko Beijing,Ujerumani ilitokea nafasi ya 5 katika orodha ya medali.Hatahivyo, ripoti ya Taasisi ya michezo (IAT) yenye kituo chake Leipzig ,imesema hakuna sababu ya kuridhika na kushangiria.

Laiti hangekuwa Britta Steffen hangeshinda medalłi za dhahabu katika hodhi la olimpik la kuogoklea katika mita 50 na 100 freestyle huko Beijing,Ujerumani ingerudi nyumbani hapo August kutoka Beijing mikono mitupu kutoka medani mbili muhimu za michezo-kuogolea na riadha ambazo kwa jumla zinachangia medali 81 za dhahabu kati ya zote 302 za Olimpik.

Kwa muujibu wa gazeti la kusini mwa Ujerumani-Suddeutsche Zeitung,Ujerumasni ni dola pekee kati ya dola 6 kuu za michezo-Marekani,China,Uingereza,Urusi na Australia ambayo hailengi moja kwa moja kunyakua medali nyingi katika mkakati wake wa spoti au katika michezo ile yenye desturi ndsefu nchini .

Ni kati ya mwezi huu tu pale kocha wa timu ya Taifa ya Ujerumani Joachim Loew na maafisa wengine wa spoti walipokwenda Ufaransa kuikagua shule mashuhuri ya dimba ya Ufaransa -football Acadamy huko Clairefontaine.

Ujerumani haina Taasisi kama hiyo na iko nyuma tangu katika mashindano ya dimba ya klabu zake hata ya kitaifa.

Ndio,Ujerumani ilimaliza wapili au makamo bingwa katika Kombe lililopita mwaka huu la Ulaya ,lakini ilizidiwa hila na mabingwa Spian mjini Vienna.Taji laoke la mwisho la kombe la ulaya lilikuwa 1996 huko Uingereza na kombe la mwisho la dunia lilinyakuliwa 1990 huko Itali.

Baada ya kustaafu kwa Michael Schumacher, Ujerumani yaweza pia isimtawaze bingwa wake wa dunia katika mbio za magari za Fomular One mwaka ujao na hata 2010.

Matumaini lakini yapo kwa kuanza mazowezi kuanzia chini na hasa kwavile Ujerumani, inaania kuandaa michezo ya olimpik ya majira ya baridi mwaka 2018.Matumaini ya kutoa mabingwa nyumbani Berlin,hapo August,mwaka huu katika ubingwa wa dunia wa riadha yapo,labda kwa kuwa mashindano yanafanyika nchini.

Kombe la CECAFA likikaribia kuanza huko Kampala,Uganda kwa timu za Taifa ,kombe la vijana la Afrika litaaniwa nchini Ruanda kuanzia januari 18-Febriari mosi.Kundi A wanatamba wenyeji rwanda,simba wa nyika Kameroun,Black Stars Ghana na Mali.Kundi B-kuna Misri,Ivory Coast,Nigeria na Bafana B afana -Afrika kusini.

Likianza tu kombe hilo la vijana, Afrika itamchagua mwanasioka wake wa mwakya -(African footballer of the year) katika sherehe maalumu mjini Dakar,Senegal:Mastadi waliofika finali ya kinyanganyiro cha taji hilo ni Mohammed Aboutraika na mwenzake Amr Zaki wa Misri,Emmanuel Adebayor wa Togo, Dididier Drogba Cortze d*ivore pamoja na Michael Essien wa Ghana.

Januari 30 firimbi italia kuanzisha duru ya kwanza ya kombe la Afrika la klabu bingwa ambamo mabingwa wa Tanzania Young Africans wana miadi Etoile d- Or Mirontsy ya Comoro wakati wenzao Miembeni ya Zanzibar watapambana na Monomotapa ya zimbabwe.Mabingwa watetezi Al Ahly Tripoli ya Libya ina miadi na Polisi ya Nigeria.Motema Pembe ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo wataumana na Mangasport ya Gabon-miongoni mwa mapam,bano kadhaa ya duru ya kwanza.

Juni, itakua asie na mwana aeleke jiwe na asie na mguu atie gongo-mkutano Afrika Kusini-kombe la mashirikisho litafungua pazia la Kombe la dunia 2010.

Kabla ya firimbi kulia miezi 6 kutoka sasa,Saumu Mwasimba anawajulisha ni timu gani kuzitazamia uwanjani:Kombe la CECAFA -Challenge Cup linaanza jumatano hii mjini kampala,Uganda na Zanzibar imeondoka leo kuelekea Kampala.Taifa Stars,Tanzania bara itaondoka jumatano .