1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KABUL:Taliban wadai kuhusika na shambulio lililokusudiwa kumlanga Cheney

28 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCNz

Msemaji wa Taliban nchini Afghanstan amedai kuhusika na shambulio la bomu lililotokea hapo jana nje ya kambi ya wanajeshi wa Marekani karibu na mji wa Kabul.

Msemaji huyo ameongeza kusema kwamba shambulio hilo lilidhamiriwa kumuua Makamu war ais wa Marekani Dick Cheney aliyekuwa ndani ya eneo hilo.

Hata hivyo bwana Cheney alinusurika na shambulio hilo ambalo lilifanywa na mripuaji wa kujitoa muhanga.

Watu kiasi 14 waliuwawa katika shambulio hilo na wengine wengi kujeruhiwa.

Mjini Washington Marekani msemaji wa Ikulu ya White House Tony Snow alisema shambulio hilo halimaanishi kwamba wataliban wananguvu nchini humo.Makamu war ais Cheney ameshaondoka Afghanstan baada ya kuwa na mazungumzo na rais Hamid Karzai juu ya usalama nchini humo.