1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KABUL:Mateka 22 waliosalia bado wako hai

27 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBeg

Mateka 22 wa Korea Kusini wanaosalia ambao bado wanazuiliwa na kundi la Taleban bado wako hai saa kadhaa baada ya muda wa mwisho uliowekwa na kundi hilo kupita.kwa mujibu wa msemaji wa kundi la Taleban Qari Mohammad Yousouf bado mazungumzo yanaendelea na hawatatoa vitisho zaidi kwani serikali imewathibitishia kuwa wana nia ya kutafuta suluhu kupitia mazungumzo. Marajudin Pathan ni Gavana wa jimbo la Ghazni kunakofanyika mazungumzo hayo.

Kundi la Taleban lilimuua kiongozi wa kundi la wahudumu 23 wa kanisa la Presbiteri nchini Korea Kusini walipokuwa msafarani kuelekea mjini Kabul.Mshauri wa rais wa masuala ya usalama wa kitaifa nchini Korea Kusini Baek Jong-chun yuko nchini Afghanistan kuongeza msukumo mazungumzo hayo ya kujaribu kutafuta suluhu.Raia mmoja wa Ujerumani pamoja na wengine 4 wa Afghanistan walitekwa kwenye visa tofauti bado wanazuiliwa.