KABUL: Watu 3 wapoteza maisha katika shambulio la bomu
16 Juni 2007Matangazo
Hadi watu 3 wameuawa kwa mripuko wa bomu lililotegwa ndani ya gari,katika mji mkuu wa Afghanistan,Kabul.Shambulio hilo pia liliwajeruhi watu wengine 5 baada ya mshambulizi aliejitolea muhanga kujiripua karibu na msafara wa magari ya vikosi vya NATO vinavyolinda amani nchini Afghanistan.Wanamgambo wa Kitaliban wamedai kuwa wao ndio waliohusika na shambulizi hilo.