KABUL : Taliban yashambulia wanajeshi wa Ujerumani
1 Septemba 2007Matangazo
Wanamgambo wa Taliban wamedai kuhusika na shambulio dhidi ya wanajeshi wa kulinda amani wa Ujerumani katika mji mkuu wa Afghanistan Kabul.
Msemaji wa kikosi cha kimataiaa cha usaidizi wa usalama ISAF kinachoongozwa na Umoja wa Kujihami wa Mataifa Magharibi NATO amesema mshambuliaji wa kujitolea muhanga maisha amelibamiza gari lake na msafara wa jeshi la Ujerumani Bundeswehr karibu na uwanja wa ndege wa Kabul.
Wanajeshi wawili wa Afghanistan wameuwawa katika shambulio hilo wakati mwanajeshi mmoja wa Ujerumani amejeruhiwa kidogo.
Katika shambulio jengine la roketi kwenye kambi ya jeshi la Marekani katika jimbo la Kunar mashariki mwa Afghanistan takriban raia 10 inaripotiwa kuwa wameuwawa.