1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Kabul. Taleban wawaachilia huru wanawake wawili.

Wanamgambo wa Taliban wamewaacha huru mateka wawili wanawake kati ya mateka 21 waliokuwa wamebaki wa Korea ya kusini ambao hadi sasa wanawashikilia nchini Afghanistan.

Msemaji wa Taliban amewaambia waandishi wa habari kwa simu kuwa wanawake hao wamekabidhiwa kwa shirika la msalaba mwekundu kati ya majimbo ya Ghazni na Zabul. Wataliban wamewauwa mateka wawili wanaume na wanatishia kuwauwa mateka waliobaki iwapo idadi kama hiyo ya wafungwa wa Taliban waliko gerezani hawataachiwa huru kwa kubadilishana na hao.

Wakati huo huo katika mazungumzo kwa njia ya simu mtu mmoja ambaye amejitambulisha kuwa ni Mjerumani anayeshikiliwa mateka nchini Afghanistan kwa zaidi ya wiki tatu sasa amesema kuwa waliomteka nyara wanataka kumuua. Mtu huyo amesema kuwa ni mgonjwa na ameiomba serikali ya Ujerumani kusaidia kupata kuachiliwa.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com