Kabul. Raia wanane wauwawa na majeshi ya Marekani. | Habari za Ulimwengu | DW | 05.03.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Kabul. Raia wanane wauwawa na majeshi ya Marekani.

Katika eneo la mashariki ya Afghanistan , maelfu ya watu wameandamana katika mji wa Jalalabad dhidi ya kuuwawa kwa raia wapatao wanane ambao wanasema walishambuliwa kwa makusudi na wanajeshi wa Marekani. Watu zaidi ya 35 wamejeruhiwa, kufutia kile maafisa wa kijeshi walichosema kuwa ni shambulio lisililokuwa la kawaida.

Maafisa wamesema majeshi ya Marekani yalirejesha mashambulizi baada ya mlolongo wa magari yao kushambuliwa na mtu aliyejitoa muhanga katika gari na kufuatiwa na mashambulizi ya risasi kutoka maeneo matatu tofauti. Majeshi ya Marekani na yale ya muungano yameahidi kufanya uchunguzi kuhusiana na tukio hilo, lakini pia wanasisitiza kuwa wanamgambo huenda wanahusika na vifo hivyo.

Kwingineko nchini humo, wanajeshi wawili wa Uingereza wameripotiwa kuwa wameuwawa katika mapigano kusini mwa jimbo la Helmand.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com