1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KABUL: Musharraf ahudhuria kikao cha mwisho cha wazee wa kikabila

12 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBZv

Rais Parvez Musharraf wa Pakistan ameliambia baraza la wazee wa kikabila kwamba kuendelea kuwepo kundi la Taliban katika maeneo ya mpakani mwa Afghanistan na Pakistan kunazuia maendeleo ya kiuchumi ambayo yangezifaidisha nchi hizo katika ulimwengu wa sasa wa utandawazi.

Awali jenerali Musharraf alikutana na mwenyeji wake rais Hamid Karzai kabla ya viongozi hao kuelekea katika kuufunga mkutano wa siku nne uliojadili hatari za makundi ya Taliban na Al Qaeda yanayoendelea kukua.

Mazungumzo hayo yalihudhuriwa na takriban washirikai 700 wakiwemo wajumbe, wazee wa makabila na viongozi mbali mbali kutoka pande zote mbili za Pakistan na Afghanistan.

Wakati huo huo askari watatu wa NATO na makalimani wao wameuwawa katika shambulio la bomu katika mkoa wa Nangarhar mashariki mwa Afghanistan leo hii.

Wapiganaji wa Taliban wamekiri kuhusika na shambulio hilo.Mfululizo wa mashambulio ya Taliban umewauwa takriban raia 29 katika maeneo mbali mbali nchni Afghanistan.

Askari wengine wawili wa kikosi cha NATO pia waliuwawa katika maeneo ya kusini na mashariki mwa Afghanistan.