KABUL: Maiti za askari watatu wa Ujerumani kurejeshwa nchini kwa mazishi | Habari za Ulimwengu | DW | 17.08.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

KABUL: Maiti za askari watatu wa Ujerumani kurejeshwa nchini kwa mazishi

Ibada ya wafu imefanywa kwa ajili ya askari watatu wa Ujerumani waliouwawa juzi Jumatano kwenye shambulio la bomu lililokuwa limetegwa kando ya barabara nchini Afghanistan. Maiti za askari hao zinatarajiwa kurejeshwa hapa nchini kwa mazishi.

Sambamba na hayo, mateka wawili wanawake wa Korea Kusini waliokuwa wakizuiliwa na wanamgambo wa kundi la Taliban nchini Afghanistan, wamewasili nyumbani hii leo.

Kim Gi - Na na Kim Kyung - Ja walionekana wamejawa na hofu na wakiwa wameathirika kisaikolojia, wakati walipowasili katika uwanja wa ndege wa Incheon magharibi mwa mji mkuu, Seoul.

Mateka wengine 19 wa Korea Kusini bado wanazuiliwa na kundi la Taliban nchini Afghanistan na wanadiplomasia wa Korea Kusini bado wanaendelea na juhudi za kuwaokoa.

Mateka wawili wa Korea Kusini waliuwawa na wanamgambo wa Taliban wakati serikali ya Afghanistan iliposhindwa kutimiza masharti yao.

Wanamgambo wa Taliban bado wanamzuilia mhandisi Mjerumani wa umri wa miaka 62, aliyetekwa nyara yapata mwezi mmoja uliopita.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com