1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

KABUL: Karzai - Maisha ya Waafghanistan si rahisi

23 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBp1

Rais Hamid Karzai wa Afghanistan,amevilaumu vikali vikosi vya NATO,kwa sababu ya idadi kubwa ya raia wanaouawa katika kile alichokiita „operesheni za uzembe“.Karzai amesema,vikosi vya NATO havijawasiliana na serikali ya Afghanistan kuhusu operesheni hizo.

Akasema,pindi hali hiyo itaendelea,basi ushindi wa vita dhidi ya ugaidi utakuwa hatarini.Amesema, kutokuwepo kwa ushirikiano na uratibu pamoja na serikali,kumesababisha idadi kubwa ya wahanga wa kiraia.Karzai amesema,maisha ya Waafghanistan,si rahisi.Akaendelea kusema kuwa haiwezekani kabisa kustahmili kuona wahanga wa kiraia.Ama hatua za kuanzisha ushirikiano na uratibu zichukuliwe,au Afghanistan itajiamulia yenyewe kuhusu suala hilo.