1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Juhudi za upatanishi zashika kasi nchini Kenya

Oummilkheir6 Januari 2008
https://p.dw.com/p/Cl6c

Nairobi/London:

Naibu waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani anaeshughulikia masuala ya Afrika bibi Jendayi Frazer anaendelea na juhudi zake za upatanishi mjini Nairobi.Mwanaadiplomasia huyo anaetazamiwa kuisalia Kenya hadi kesho usiku,amepanga kukutana tena na wakuu wa pande mbili zinazohasimiana,baada ya mazungumzo yake ya jana pamoja na rais Kibaki na kiongozi wa upande wa upinzani wa ODM Raila Odinga.Kwa mara nyengine tena Raila Odinga amelikataa pendekezo la kuundwa serikali ya umoja wa taifa.”Akizungumza na waandishi habari Raila Odinga amesema “hawana kiu cha madaraka,wanataka ufumbuzi wa kudumu kwa mzozo uliopo.”Wakati huo huo waziri mkuu wa Uengereza Gordon Brown amezungumzia “fursa nzuri ya kupatikana suluhu nchini Kenya.Rais John Kufour wa Ghana,mwenyekiti wa sasa wa umoja wa Afrika asnatazamiwa kuwasili Nairobi siku mbili kutoka sasa.