Juhudi za uokoaji wa maafa ya maporomoko nchini Uganda zaendelea
3 Machi 2010Matangazo
Hata hivyo, kutokana na ugumu wa eneo yalikotokea maafa hayo, magari na vifaa vikubwa vya uokozi hayawezi kufika, hivyo waokozi wamekuwa wakitumia mikono kufukua watu waliofunikwa na matope hayo. Inakadiri kuwa zaidi ya watu mia tatu wamefunikiwa , huku maiti kiasi ya 80 mpaka sasa ndizo zilizopatikana.
Mwandishi wa Kampala Leyla Ndinda amekwenda katika eneo hilo la maafa, na Aboubakary Liongo amezungumza naye muda mfupi tu uliyopita akiwa anapanda mlima kuelekea katika vijiji vilivyofikwa na maafa hayo.
Mwandishi:Aboubakary Liongo
Mhariri:Othman Miraji