1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Juhudi za kuhifadhi uoto wa asili na misitu Shinyanga

3 Julai 2015

NGITILI ni eneo maalumu ambalo linatengwa kwa ajili ya kuhihadhi uoto wa asili na misitu. Hizi ni juhudi ambazo zinafanywa katika nchi za Afrika ili kuweza kukabiliana na tatizo la mabadiliko ya tabia nchi hasa ukame.

https://p.dw.com/p/1Fs23
Tansania Projekt Baumpflanzung Reduzierung Karbondioxid
Veronica Natalis (kushoto) na Mzee Mzee Maxmillian Simangu, mkulima na mkazi wa kijiji cha Manyada mkoani Shinyanga, TanzaniaPicha: DW/V. Natalis

Nchini Tanzania katika mkoa wa Shinyanga zaidi ya wakazi 50 wamefanikiwa kuhifadhi NGITILI baada ya mradi wa majaribio wa kupunguza uzalishaji wa hewa ukaa unaotokana na ukataji miti hovyo na uharibifu wa misitu MKUHUMI kufanyika kwa majaribio kuanzia mwaka 2009 hadi 2014 unaotekelezwa kwa ubia kati ya Shirika la Kuhifadhi Misitu ya Asili Tanzania (TFCG) na Mtandao wa Jamii wa Usimamizi wa Misitu Tanzania (MJUMITA) kuwapa elimu wananchi hao jinsi ya kuhifadhi NGITILI.

Mradi huo umeonekana kuwa na mafanikio baada ya NGITILI hizo kuonekana kufanikiwa kupunguza kiwango cha hewa ukaa angani.

Mpango wa kupunguza uzalishaji hewa ukaa unaotokana na ukataji miti hovyo na uharibifu wa misitu yaani MKUHUMI, umetekelezwa kwa majaribio kwa miaka mitano kuanzia mwaka 2009-mpaka mwaka 2014 na umetekelezwa kwa ubia kati ya Shirika la Kuhifadhi Misitu ya Asili Tanzania (TFCG) na Mtandao wa Jamii wa Usimamizi wa Misitu Tanzania yaani Mjumita. Miongoni mwa mikoa ambayo imetekeleza mradi huo wa majaribio nchini Tanzania ni mkoa wa Shinyanga ambapo moja kati ya utekelezaji wake ni uhifadhi wa NGITILI.

Katika kipindi hiki cha Mtu na Mazingira, mwandishi wetu wa Shinyanga, Veronica Natalis, anaangalia juhudi za uhifadhi wa Ngitili.

Kusikiliza makala bonyeza alama ya spika za masikioni hapo chini

Mwandishi:Veronica Natalis

Mhariri:Josephat Charo