1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Juhudi za kubadilishana wafungwa kati ya Israel na Palastina

Jerusalem:

Israel imepokea orodha ya majina ya wafungwa wa kipalastina wanaobidi kuachiwa huru ili kubadilishana na mwanajeshi wa kiisrael Gilad Schalit.Afisa wa ngazi ya juu katika serikali ya Israel amesema katika orodha hiyo kuna majina ya mamia ya wapalastina waliohusika na mauwaji ya wanajeshi au raia wa kiisrael.Gilad Schalit alitekwa nyara na wapalastina huko Gaza,mwezi June mwaka jana.Inasemekana orodha hiyo ya majina ya wafungwa ilikabidhiwa kwanza Misri,inayojaribu kupatanisha tangu miezi kadhaa sasa katika mzozo huo.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com