1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

JOHANNESBURG: Watu 19 wafa kutokana na mioto

30 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBdi

Watu takriban 19 wameuwawa na makaazi yasiyopungua 320 kuharibiwa kufuatia mioto iliyozuka kwenye misitu kaskazini mashariki mwa Afrika Kusini.

Maafisa wa Afrika Kusini wamesema leo kuwa watu 13 walikufa katika maeneo ya mkoa wa KwaZulu Natal huku wazima moto sita wakifa katika mkoa jirani wa Mpumalanga mwishoni mwa juma.

Taarifa iliyotolewa na serikali ya jimbo la KwaZulu Natal imesema maelfu ya nguruwe, kondoo, ng´ombe na mbuzi aidha waliteketea hadi kufa au ilibidi wachinjwe kufuatia majeraha mabaya ya moto.