JOHANNESBURG: Mwanamuziki Lucky Dube ameuawa na majambazi | Habari za Ulimwengu | DW | 20.10.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

JOHANNESBURG: Mwanamuziki Lucky Dube ameuawa na majambazi

Lucky Dube,mwanamuziki mashuhuri wa midundo ya reggae wa Afrika Kusini, amepigwa risasi na kuuawa mbele ya watoto wake mjini Johannesburg.Dube aliekuwa na umri wa miaka 43 aliauwa na majambazi waliojaribu kumnyanganya gari lake.

Dube alitembelea nchi mbali mbali duniani,akiimba kuhusu matatizo ya kijamii.Katika maisha yake kama muimbaji,ametunukiwa zaidi ya zawadi 20 nyumbani na nchi za kigeni.

Rais Thabo Mbeki amesema,wananchi wote wanapswa kufanya kazi pamoja kukomesha uhalifu Afrika Kusini-nchi yenye idadi kubwa kabisa ya mauaji duniani.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com