JOHANNESBURG : Mahkama yaunga mkono kesi dhidi ya Zuma | Habari za Ulimwengu | DW | 08.11.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

JOHANNESBURG : Mahkama yaunga mkono kesi dhidi ya Zuma

Mahkama nchini Afrika Kusini leo hii imeipa uhai kesi ya rushwa iliokwama dhidi ya makamo wa rais wa zamani wa nchi hiyo Jacob Zuma ambaye yuko mstari wa mbele kuwania nafasi ya kukiongoza chama tawala nchini humo cha ANC.

Mahkama Kuu ya Rufaa imeungana na waendesha mashtaka kwa kutowa hukumu kwamba nyaraka zilkizokamatwa kutoka kwa Zuma na wakili wake katika msako wa polisi zinaweza kutumika katika kesi za rushwa dhidi yake katika kipindi cha usoni.

Mahkama Kuu imetenguwa hukumu za mahkama ndogo kwamba nyaraka hizo zilikuwa haziwezi kutumika kwa ushahidi kwa sababu polisi walikuwa hawana hati sahihi za upekuzi.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com