JOHANESSBURG : Mshauri wa Zuma kuhukumiwa Jumatatu | Habari za Ulimwengu | DW | 05.11.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

JOHANESSBURG : Mshauri wa Zuma kuhukumiwa Jumatatu

Mshauri wa zamani wa Rais wa Afrika Kusini aliyetimuliwa madarakani Jacob Zuma anakabiliwa na hukumu hapo kesho Jumatatu kwa rufaa yake dhidi ya kupatikana na hatia ya rushwa hukumu ambayo wachambuzi wa mambo wanasema yumkini ikajenga au kubomowa nafasi ya Zuma kuwa rais wa nchi hiyo.

Mfanya biashara Shabir Shaikh alipatikana na hatia ya rushwa na udanganyifu baada ya hakimu kugunduwa kwamba alikuwa na uhusiano wa rushwa na Zuma hukumu ambayo ilipelekea Rais Thabo Mbeki kumtimuwa Zuma ambaye wakati fulani alionekana kuwa ndio mrithi wake.

Waendesha mashtaka baadae walimshtaki Zuma mwenyewe kwa kupokea hongo kuhusiana na mikataba ya silaha lakini hakimu aliitupilia mbali kesi hiyo na serikali kuja kuadhirika vibaya kutokana na kushindwa kwake.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com