1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Jeshi la Ujerumani lalaumiwa

Oumilkher Hamidou7 Septemba 2009

Kansela Angela Merkel ahimiza uchunguzi ufanywe na NATO kujua yaliyotokea

https://p.dw.com/p/JTvG
Wanajeshi wa Ujerumani huko Kundus-AfghanistanPicha: AP

Lawama dhidi ya jeshi la shirikisho Bundeswehr hazijapungua."Wamepitisha uamuzi kwa pupa-walipoamrisha usiku wa alkhamisi kuamkia ijumaa iliyopita, malori mawili yaliyosheheni mafuta yaripuliwe kwa mapomu huko Kunduz,kaskazini mwa Afghanistan".Kwasababu hakujakua na uhakika kama raia wa kawaida hawajakuwepo karibu na malori hayo.Kwa mujibu wa ripoti iliyotangazwa na jeshi la shirikisho la jamhuri ya Ujerumani-Bundeswehr ijumaa iliyopita,shambulio hilo liligharimu maisha ya waasi wa Taliban tuu.Ripoti ya jana ya gazeti la Washington Post inazisuta hoja hizo na kudai dazeni mbili ya raia wameangukia pia mhanga wa hujuma hizo.

Maoni yanatofautiana linapohusika suala la kile kilichotokea hasa usiku wa alkhamisi kuamkia ijumaa huko Kundus ,kaskazini mwa Afghanistan.Lakini licha ya ripoti zisizo bayana,kisa hicho kilihanikiza mtindo mmoja mwishoni mwa wiki.Kwasababu jana gazeti la Washington Post liliripoti kwamba katika hujuma hizo watu 120 wameuwawa na si chini ya dazeni moja walikua raia wa kawaida.

Hadi wakati huu yaliyokua yakijulikana ni haya yafuatayo:

Alkhamisi iliyopita waasi waliyateka nyara malori mawili yaliyo sheheni mafuta karibu na kambi ya wanajeshi wa Ujerumani,

Bundeswehr huko Kundus.Waasi walikwama walipotaka kuuvuka mto Kundus,umbali wa kilomita 6 karibu na kambi ya wanajeshi wa Ujerumani.Saa chache baadae,mkuu wa shughuli za vikosi vya Bundeswehr,kanali Georg Klein akaamuru malori hayo yaliyosheheni mafuta yapigwe mabomu.Yakaripuka na aliyekua karibu na hapo hakua na nafasi yoyote ya kusalimika.Kwa mujibu wa Bundeswehr,raia wa kawaida hawajaangukia mhanga wa mashambulio hayo.

Akizungumzia juu ya uamuzi wa kanali George Klein,waziri wa ulinzi wa serikali kuu ya Ujerumani Josef Jung alisema :

"Kutokana na hali ya kutisha inayowakabili wanajeshi wetu,nnaweza nikauelewa vizuri uamuzi uliopitishwa na uongozi wetu na nnauunga mkono pia.Na ndio maana nnahisi tunabidi kufanya kila liwezekanalo linapohusika suala la uchunguzi,lakini tusisahau pia wanajeshi wetu wanajikuta katika hali ya hatari kabisa katika eneo hilo.Na ndio maana kila la kufanya lifanywe kuwaepushia hatari wanajeshi wetu."

Katika wakati ambapo waziri wa ulinzi Josef Jung anazungumzia suala hilo,lawama dhidi ya Ujerumani zimekua zikihanikiza katika kila pembe ya dunia.Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Ufaransa Bernard Kouchner amelitaja shambulio hilo kua "kosa kubwa".Waziri mwenzake wa Sweeden Carl Bildt amesema "ingekua bora kama kisa hicho kingeshughulikiwa vyengine."

Kisa hicho kimezidishwa makali na gazeti la Washington katika toleo lake la jana.Gazeti hilo linakosoa miongoni mwa mwengineyo duru zilizofuatwa na uongozi wa jeshi la Ujerumani katika kupitisha uamuzi huo.Ripoti ya Washington Post inaonyesha kana kwamba lilikua kosa kuziamini duru na kuamua malori yaripuliwe.

Deutschland Großbritannien Angela Merkel und Gordon Brown zu Afghanistan
Kansela Angela Merkel katika mkutano na waandishi habari pamoja na waziri mkuu wa Uengereza Gordon BrownPicha: AP

Kansela Angela Merkel ametoa mwito uchunguzi ufanywe haraka.Amesema wazi :

"Kwamba serikali kuu ya Ujerumani na mie binafsi tunataka paundwe tume ya uchunguzi ya NATO ili kuchunguza kisa hiki haraka,kujua nini hasa kimetokea na kama raia wameangukia mhanga wa mashambulio hayo.Mnajua,mkakati wetu unalenga kutafuta na kupata imani ya wananchi."

Jana kansela Angela Merkel na waziri mkuu wa Uengereza Gordon Brown wametoa mwito mkutano wa kimataifa kuhusu Afghanistan uitishwe kabla ya mwaka huu kumalizika .Lengo la mkutano huo ni kuwahimiza waafghani wawajibike zaidi nchini mwao.

Mwandishi:Ballweg,Silke/Hamidou Oummilkheir

Mhariri:M.Abdul Rahman