1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

JERUSALEM.Olmert na Abbas kukutana tena

25 Oktoba 2007
https://p.dw.com/p/C7Cz

Viongozi wa Israel na Palestina watakutana kesho ili kujaribu kuondoa tofauti kuhusu hati inayokusudiwa kuwasilishwa kwenye mkutano juu ya kuundwa nchi ya wapalestina utakaofanyika Maryland, chini ya udhamini wa Marekani.

Habari zinesema hatua imepigwa baina ya wajumbe wa pande mbili hizo juu ya maudhui ya hati ya pamoja kwa ajili ya mkutano huo utaotarajiwa kufanyika kati ya mwezi wa novemba na desemba.