1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

JERUSALEM: Waziri mkuu wa Israel, Ehud Olmert, tayari kwa mazungumzo na Palestina na Lebanon

17 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD28

Waziri mkuu wa Israeli, Ehud Olmert, aliliambia bunge kwamba yuko tayari kukutana kwa mazungumzo na rais wa Palestina, Mahmoud Abbas. Ehud Olmert, alimtolea mwito pia waziri mkuu wa Lebanon, Fouad Siniora, kukubali mazungumzo ya ana kwa ana kwa ajili ya amani kati ya pande hizo mbili. Rais wa Israeli, Moshe Katsav, yeye hakushiriki katika kikao hicho cha bunge, ikiwa ni siku moja baada ya polisi kupendekeza afunguliwe mashtaka ya ubakaji na udanganyifu. Polisi imesema ilikusanya ushahidi wa kutosha dhidi ya Moshe Katsav.

Hata hivyo hatua ya kufunguliwa mashtaka au laa itachukuliwa na mwanasheria mkuu, Meni Mazuz. Rais Moshe Katsav alikana madai hayo ya polisi.