1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Jerusalem: Olmert kukutana na Abbas

16 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBi7

Waziri mkuu wa Israel Ehud Olmert na rais Mahmoud Abbas wa Palestina watakutana Jerusalem leo kuzungumzia mipango ya Israel kuisaidia mamlaka ya wapalestina katika ukingo wa magharibi. Katika hatua ya kwanza iliotangazwa na Israel jana, imesema haitawalenga tena wapiganaji wa kundi la Fatah, ikiwa watasitisha mashambulio yao dhidi ya Israel. Marekani inamtaka Bw Olmert aanze tena mazungumzo na Abbas baada ya kundi pinzani la Hamas kutwaa mamlaka kwa nguvu katika ukanda wa Gaza.