JERUSALEM : Olmert kukutana na Abbas leo
15 Aprili 2007Waziri Mkuu wa Israel Ehud Olmert na Rais Mahmoud Abbas wa Palestina wanakutana mjini Jerusalem leo hii lakini wasaidizi wao hawaweki matumaini makubwa ya kufikiwa kwa uvumbuzi wa aina yoyote ile.
Mazungumzo hayo ni ya kwanza kati ya Olmer na Abbas tokea walipokubaliana wakati wa ziara ya waziri wa mambo ya nje wa Marekani Condoleezza Rice mwezi uliopita kukutana kila baada ya wiki mbili.
Wasaidizi wa Olmert wamesema amejiandaa kujadili na Abbas miundo ya kisheria,kiuchumi na kiserikali ya serikali ya Palestina ya kipindi cha usoni.
Lakini maafisa wa Israel wanasema masuala matatu makuu ya kufafanuwa mipaka ya taifa la Palestina,hadhi ya mji wa Jerusalem na hatima ya wakimbizi wa Kipalestina hayatakuwemo kwenye agenda.