1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

JERUSALEM: Olmert ataka kukutana na viongozi wa kiarabu

30 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCEE

Waziri mkuu a Israel, Ehud Olmert, amesema yuko tayari kuzungumza na Saudi Arabia na mataifa mengine ya kiarabu yasiyo na msimamo mkali wa kidini. Olmert anaamini amani baina ya Israel na Palestina huenda ikapatikana katika kipindi cha miaka mitano ijayo.

Katika mahojino yake yaliyochapishwa leo na magazeti ya Israel, Ehud Olmert amesema mpango wa amani ulioidhinishwa na viongozi wa kiarabu mjini Riyahd, Saudi Arabia huenda ukasaidia kuyaendeleza mazungumzo ya kutafuta amani katika siku za usoni.

Mpango huo unaipa Israel uhusiano wa kawaida na mataifa ya kiarabu ikiwa itaihama ardhi iliyoiteka wakati wa vita vya Mashariki ya Kati vya mwaka wa 1967, kuundwa kwa taifa huru la Wapalestina na suluhisho la haki kwa Wapalestina waliopoteza makazi yao wakati wa kuundwa kwa taifa la Israel mnamo mwaka wa 1948.