JERUSALEM: Condolezza Rice akutana na Ehud Olmert | Habari za Ulimwengu | DW | 15.01.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

JERUSALEM: Condolezza Rice akutana na Ehud Olmert

Waziri wa mashauri ya kigeni wa Marekani Condoleezza Rice amekutana na waziri mkuu wa Israel, Ehud Olmert mjini Jerusalem leo asubuhi. Mazungumzo yao yametuwama juu ya kumuimarisha rais wa Palestina, Mahmoud Abbas, dhidi ya wanamgambo katika maeneo ya wapalestina.

Waziri Olmert anatarajiwa kuonya kwamba kuundwa kwa serikali ya umoja wa matafa nchini Palestina ambayo haitalitambua taifa la Israel na kukomesha machafuko kutamaliza msaada wa Israel kwa rais Abbas.

Condoleezza Rice alikutana na rais Abbas jana mjini Ramallah baada ya kukutana na waziri wa mambo ya kigeni wa Israel, Tzipi Livni juzi Jumamosi. Bi Rice amesema Marekani imejitolea katika juhudi za kutafuta amani Mashariki ya Kati.

´Marekani imejitolea kwa dhati kutafuta njia za kuuharakisha mpango wa amani ya Mashariki ya Kati. Mpango huo unatambuliwa kimaitaifa kama kielelezo cha kundwa kwa mataifa ya Israel na Palestina na tuna jukumu la kuutekeleza kikamilifu.´

Marekani inakabiliwa na shinikizo kutoka kwa washirika wake barani Ulaya na mataifa ya kiarabu ijihusishe zaidi katika kuutanzua mzozo wa Israel na Palestina.

Condoleezza Rice anataka msaada wa mataifa ya kairabu kumsaidia rais Abbas na kuiimarisha Irak katika ziara yake itakayompeleka Misri, Saudi Arabia, Kuwait, Ujerumani na Uingereza.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com