1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiJapan

Japan yasitisha msaada wa fedha kwa shirika la UNRWA

Saumu Mwasimba
29 Januari 2024

Japan imejiunga na nchi chungunzima za Magharibi kusitisha kwa muda msaada kwa shirika la Umoja wa Mataifa la kuwasadia wakimbizi wa Kipalestina - UNRWA.

https://p.dw.com/p/4bmnj
Shirika la Umoja wa Mataifa la kuwasadia wakimbizi wa Kipalestina - UNRWA

Wizara ya mambo ya kigeni ya Japan imesema jana Jumapili kwamba msaada wake wa kifedha kwa shirika hilo unasitishwa kwa kipindi hiki na kuongeza kwamba inawasiwasi mkubwa kuhusu madai ya kuhusika wafanyakazi wa shirika hilo katika mashambulio ya kigaidi dhidi ya Israel yaliyofanywa October 7.

Nchi nyingi zikiwemo, Marekani,Ujerumani na Ufaransa zimechukuwa hatua kama hiyo.

UNRWA linahusika kutoa msaada wa kibinadamu katika maeneo ya mamlaka ya Wapalestina.Wafanyakazi wake 12 wanadaiwa walihusika katika mashambulio ya kundi la Hamas dhidi ya Israel ya tarehe 7 mwezi Oktober.

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema uchunguzi utafanyika na hatua zitachukuliwa.

Waziri mkuu wa Palestina Mohammad Shtayyeh amelaani tuhuma za Israel dhidi ya UNRWA.